Shilole aka Shi Shi Baby amesema anaachia wimbo wake mpya alioupa jina ulioandaliwa na producer Nha Real.Akiongea na mwandishi wa blogu hii Shishi baby amesema,anaona huu ni muda muafaka wa yeye kuachia wimbo mpya kwaajili ya mashabiki wake ambao wamekuwa wakisubiri muziki mzuri kutoka kwake.
Shilole ameongeza kusema,wimbo ni mzuri na amefanya kazi nzuri kama ilivyo ada yake na ukizingatia amefanya na producer wanayesikilizana,Nah Real.
Shilole anaachia wimbo huo mpya ikiwa ni siku chache tangu atoke Africa kusini kwa ziara ya kimuziki ambapo aliwachengua vilivyo watanzania nawapenzi wa muziki wa kizazi kipya waishio mji wa Cape Town.
Shihi baby pia amesema anaachia wimbo huo na wakati watu wakiburudika,yeye anaenda katika ziara ya muziki huko Belgium ambako atatumbuiza katika miji mitatu,ijumaa tarehe 28 atakuwa Brussel na jumamosi tarehe 29 atakuwa Hoeilaat.
0 comments:
Post a Comment