Baada ya habari za Chris kuwa na mtoto,aliyekuwa mpenzi wake, Karrueche amesema hamuhitaji tena katika maisha yake.Mtandao wa Hollywoodlife.com umeripoti habari hiyo.
Karrueche Tran, 26, amesema haitaji tena mahusiano na Chris Brown 25 baada ya kile alichokiita ni kama mchezo wa kuigiza baada ya kusikia habari juu ya mpenzi wake huyo kupata mtoto na mwanamke mwingine.Chris imetangazwa kapata mtoto ambaye sasa ana umri wa miezi 9 na mwanamitindo wa zamani,Nia Guzman, 31.
Karrueche Tran amekuwa katika mahusiano na Chris Brown kwa takribani miaka 4 ambapo amepitia mengi ikiwamo ya Chris kumtaka akubali kuwa naye huku akijihusisha na Rihanna ( a love triangle ) lakini kwa hili la Chriss kupata mtoto na mwanamke mwingine wakiwa katika mahusiano,linaonekana kumkera na hata kufikia kusema hamuhitaji tena.
0 comments:
Post a Comment