Mama mzazi wa Tracy Morgan,Alicia Warden alishangazwa na kitendo cha kuzuiwa kuingia hospitali kumjulia hali mwanawe aliyelazwa.
Alicia Warden
ambaye hana mahusiano azuri na mwanawe ambaye ni muigizaji maarufu wa filamu Hollywood,Tracy Morgan aliuambia mtandao wa TMZ kwamba mbali ya kuziwa kuingia hospitali hapo,hakuna mtu aliyempigia kutaarifu kuhusu mwanae kupata ajali mbaya ya gari bali aliona habari kwenye TV.
Mamam huyo anasema alipokwenda hospitali hapo alizuiwa na na walinzi na mpenzi wa Tracy Morgan,Megan Wollover.
Mama yake Tracy amaesema alirudi siku inayofuata na aliruhusiwa kumuona mwanaye kwa dakika 5 tu hawakujali kama alikwenda na mchungaji amfanyie maombi.
Morgan alishawahi kuongea mwaka 2012 kwamba yeye na mama yake hawana mahusiano mazuri na hajaonana na mama yake kwa takribani miaka 11.
Thursday, June 12, 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment