Msanii nyota wa muziki wa Pop Madonna,alianguka jukwaani wakati alipokuwa akitumbuiza katika sherehe za utoaji wa tuzo za muziki za Britts 2015.Madonna alijikwaa katika ngazi na kuaguka vibaya baada ya mchezaji densi mmoja kujaribu kutoa kofia aliokuwa amevaa mwanzoni mwa onyesho hilo lakini hatahivyo mwanamuziki huyo aliinuka na kuendelea kuimba wimbo wake Living for love.Baadaye nyota huyo mwenye umri wa miaka 56 alitoa taarifa yake akisema kuwa yuko salama na kwamba kofia yake ilikuwa ikimbana sana.
''hakuna kinachoweza kunizuia na kwamba mapemzi yaliniinua juu''aliandika katika Istangram akinukuu maneneo katika wimbo wake.
Ed Sheeran alichaguliwa kama msanii bora mwanamume wa kipekee Uingereza.Taylor Swift, alitajwa kama msanii mwanamke wa kimataifa wa kipekee. Katika sherehe hizo.
0 comments:
Post a Comment