Chris Brown alizuiwa katika mpaka wa Canada ikiwa ni masaa kadhaa kabla ya kwenda kutumbuiza katika tamasha maalumu la ziara ya muziki ya Chris Brown na Trey wakisindikizwa na Tyga .Brown alitweet, "The good people of the Canadian government wouldn't allow me entry. I'll be back this summer and will hopefully see all my Canadian fans!".
Chris Brown,Trey Songs na rappa Tyga walitakiwa kutumbuiza katika ziara yao ya muziki waliyoipa jina la Between the sheet ambalo lilipangwa kufanyika huko Montreal siku ya jumanne na siku ya jumatano ilipangwa kufanyika Toronto.Chanzo kimoja cha karibu na mastaa hao kimedai tiketi za matamasha yote hayo ziliisha.
Taarifa zaidi zinasema Canada hawapokei wageni wahalifu ama wanaokabiliwa na kesi.Chris Brow bado anakabiliwa na kesi ya kumpiga aliyekuwa mpenzi wake,Rihanna mwaka 2009 na pia anakabiliwa na kesi mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment