Ile beef kati ya Lil Wayne na ya Birdman inazidi kuchukua kasi,taarifa zinadai mastaa hao walijikuta wakiwa katika club moja ambapo rappa Lil Wayne alikuwa akifanya Club appearance jukwaani ndipo Birdman alipommwagia kinwaji kichwani.
Tukio hilo lilitokea katika club inayofahamika kama LIV nightclub huko Miami siku ya jumapili.
Shuhuda wa tukio hilo amesema alimuona Birdman amesimama pembeni ya DJ booth ya juu ya jukwaa iliyopo VIP ndipo alipoona kinywaji kimemwagwa kichwani mwa Lil Wayne.
Birdman alifanya tukio hilo japo kamera hazikufanikiwa kumnasa.
Ikumbukwe tu Weezy amemfungulia mashtaka Birdman akitaka alipwe zaidi ya dolla millioni 51 na anataka kuwa huru na kujitoa katika lebo ya Cash Money.
0 comments:
Post a Comment