Katika sherehe za utaji wa tuzo za Video Music Awards mwaka huu zitakazofanyika tarehe 30 August katika ukumbi wa Microsoft Theater huko Los Angela,rapa Kanye West ametajwa kutunukiwa tuzo malumu ya heshima ya Michael Jackso inayofahamika kama "Michael Jackson Video Vanguard Award" .
Tuzo hiyo imeshatolewa kwa mastaa wakubwa wa muziki kama Justin Timberlake, Janet Jackson na Beyoncé ambaye alitunukiwa mwaka uliopita.
Pamoa na kutajwa kutunukiwa tuzo hiyo bado rapa Kanye West hajatajwa kama atatumbuiza katika sherehe za utoaji wa tuzo za MTV Award mwaka huu japo wasanii kama Pharrell, A$AP Rocky, Macklemore na The Weeknd wametajwa kutumbuiza huku muimbaji mwenye vituko,Miley Cyrus ametajwa kuwa muongozaji wa shughuli hiyo.
Na katika habari nyingine kuna habari njema kuhusiana na star Kanye West na mkewe Kim Kardashian ambayo inahusu kushinda kesi waliyomfungulia mfanyakazi wa mtandao wa Youtube kwa kuvujisha kipande cha video ya Kanye akimvisha pete ya uchumba Kim 2013.Taarifa zinadai mtu huyo kuwalipa mastaa hao zaidi ya dola 440,000.
0 comments:
Post a Comment