Jimmy Winfrey ndiye mtu anayeshikiliwa na polisi akihusishwa na tukio la shambulio la basi la ziara alilokuwamo Lil Wayne na wenzake wa Young Money.
Bwana Jimmy Winfrey katika maelezo aliyoandika hivi karibuni mahakamani ameitaka mamlaka ya polisi nchini marekani kumkamata Birdman kwa kile alichokisema anahusika moja kwa moja kwani tukio hilo lilitokea baada ya Birdman na Lil Wayne kuingia katika ugomvi uliopelekea rappa Lil Wayne kufungua kesi ya madai ya mamilioni ya madola na kutaka kujiondoa yeye na Young Money ndani ya Cash Money.
Mwezi December, Lil Wayne kupitia akaunti yake ya Twitter aliandika kuhusu yeye na kundi lake la Young Money kujitoa Cash Money na kuifungulia Cash Money Records kesi ya madai ya dolla millioni 8.
Mwezi uliopita Birdman na Young Thug walitajwa kuhusika na tukio hilo la shambulizi dhdi ya basi la ziara ya muziki la Lil Wayne na kundi la Young Money lakini Birdaman alikanusha kuhusika na tukio hilo.
0 comments:
Post a Comment