Drake ameamua kuvunja ukimya.Rappa huyo toka Canada ambaye hivi karibuni ametokea katika kasha la jarida la The FADER pia ameongelea kuhusu mixtape yake na rappa Future ambayo wameipa jina la What a Time to Be Alive.
Mwandishi wa jarida hilo alipata nafasi ya kupiga story na Drizzy akiwa hometown kwao huko Toronto, Drake alifunguka kuhusu ishu mbalimbali ikiwemo ya tuhuma za kusemekana anaandikiwa ngoma zake ( ghostwriting ) na akaongelea kuhusu beef yake na rappa Meek Mill.
Kuhusu kuandikiwa ngoma Drake amaesema:mara nyingine huwa nakuwa na watu wengine kupata ideas nyngine na vitu vipya,hivyo huwa nawatumia watu kupata vitu vpya na vizuri tofauti na ukiwa mwenyewemwenyewe utakuwa yuleyule siku zote.Si kweli kwamba naadikiwa ila huwa tunashirikiana katika kutafuta mawazo mazuri.
Kuhusu beef yake Meek Mill amesema:ile ilikuwa sehemu katika muziki na halikuwa wazo baya kama wengi walivyochukulia.Ilikuwa sehemu pia ya kujipima japo sikupata upinzani mkubwa
Friday, September 25, 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment