Mwanamuziki maarufu Koffi Olomide amekataliawa dhamana ya kuachiliwa huru kulingana na wakili wake.
Jaji alikataa ombi lake la la kuachiliwa wakati alipowasilishwa mahakamani.Siku ya Jumatatu ,maafisa wa polisi walimkamata Olomide mwenye umri wa miaka 60 nyumbani kwake katika makaazi ya Kinshasa baada ya kupatikana katika kamera akimpiga teke mmoja wa wanenguaji wake katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta mjini nairobi.
Alirejeshwa nchini DRC kutoka Kenya kufuatia kisa hicho cha Ijumaa.
Hatua hiyo ilisababisha kufutiliwa mbali kwa tamasha lake nchini Kenya na Zambia.
Amekana mashtaka yanayomkabili.Source BBC.
0 comments:
Post a Comment