Ule msemo unaosema ukitaka kugombana na mwanaume mwenzako mzingue kuhusu pesa ama mpenzi wake umejidhihirisha pale ambapo Justin Bieber alipogeuka mbogo alipoulizwa kuhusu anayesemekana kuwa ni hasimu wake kwa sasa,The Weeknd.
Uhasimu wa wanamuziki hao nguli toka Canada Justin Bieber na The Week end umesababishwa na minong;ono ya The Weeknd kujihusisha na ex wa Justin bieber,Selena Gomez.
The pop superstar Justini Bieber Gomez alirusha kombora la kumponda The Weekend pale alipoulizwa huwa anasikiliza nyimbo zake ndipo aliposema huwa hasikilizagi muziki wa wapuuzi.
Wajuzi wa mambo wanasema pamoja na kuwa katika hali ya kutoelewana kwa Bieber na Selena lakini inaonekana bado Bieber anamuonea wivu mrembo huyo kwani hata majibu hayo inawezekana yamesababishwa na kusambaa kwa kipande cha video kikimuonyesha The Weeknd akim busu Selena nje ya mgahawa wa Santa Monica mapema mwezi huu.
0 comments:
Post a Comment