Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Wednesday, December 11, 2013

 Kanye West
Baada ya majina ya wanaowania tuzo za Grammy kutangazwa wiki iliyopita na Kanye west kuonekana katika nafasi mbilitu,rappa huyo mwenyeji wa Chicago aliamua kuwachana waandaaji hao wa tuzo zaGrammy pale alipokuwa katika "Yeezus Tour" huko Phoenix,Arizona.Kanye alionyesha kiasi gani hakuridhishwa na uteuzi huo uliompatia nafasi 2 tu ambazo ni Best Rap Album (Yeezus) na Best Rap Song (“New Slaves”).Kanye West pia amesema japo ana tuzo 21 za  Grammys,hajawahi kushinda tuzo  ya Grammy hata moja aliyowahi kushindania na msanii mwenye asili ya kizungu.
Kanye anawania tuzo ya the Best Rap Album na Drake (Nothing Was The Same), Kendrick Lamar (good kid, m.A.A.d city), Jay Z (Magna Carta Holy Grail) na Macklemore & Ryan Lewis (The Heist).Vilevile Kanye anawania tuzo ya Best Rap Song kwa track yake New Slaves,akiwania tuzo hiyo na A$AP Rocky's "F***in' Problems,” Jay-Z's “Holy Grail,” Drake's “Started From The Bottom” na Macklemore & Ryan Lewis “Thrift Shop.”
Wakati watu wa Grammy wamempatia nafasi finyu,albamu ya Kanye West  Yeezus imeteuliwa namba moja na jarida la Times katika kipengele cha Times top 10 list.Albamu hiyo ya West pia imepewa nafasi ya kwanza na jarida la Entertainment Weekly's list na kama haitoshi imeshika nafasi ya pili katika Rolling Stone's Top 10.

0 comments:

Post a Comment