Uganda imepitisha mswada unaopinga mapenzi ya jinsia moja.
Iwapo Rais Yoweri Museveni ataidhinisha sheria hiyo inamaanisha atakayepatkana na hatia atahukumiwa kifungo cha maisha gerezani.
Mswaada huo uliopitishwa na bunge siku ya Ijumaa halikadhalika inasema mtu yeyote aliye na taarifa za watu wanoshiriki mapenzi ya jinsia moja na kushindwa kuripoti habari hizo kwa maafisa wa polisi atafungwa gerezeni maisha.
Wakati hu huo bunge hilo hilo la Uganda siku ya Alhamisi liliidhinisha mswaada unaopiga marufuku maonyesho ya picha za chafu.
Mswada huo unaharamisha kitu chochote kitakachoonyesha sehemu nyeti kama vile matiti, mapaja, makalio au tabia yoyote inayozua uchu wa mapenzi.
Kufuatia kuoitishwa kwa sheri ahiyo wanaharakati wa wapenzi wa jinsia moja, mawakili na wansiasa wamewasilisha kesi mahakamani nchini Uganda kupinga sheria mpya dhidi ya mapenzi ya jinsia moja nchini humo.
Wanaharakati hao, wanasema kuwa sheria hiyo inakiuka katiba ya Uganda na kuendeleza ubaguzi na kukandamiza uhuru wa kujieleza.
Sheria hiyo ilitiwa saini na Rais Yoweri Museveni mwezi jana na imelaaniwa vikali na jamii ya kimataifa.
Rais wa Marekani Barack Obama ameitaja sheria hiyo kama hatua ya ukandamizaji kwa waganda na nchi kadhaa tayari zimetishia kuinyima Uganda msaada.

0 comments:
Post a Comment