Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Monday, December 1, 2014

Mwanamuziki mwenye sifa kedekede nchini Tanzania, Naseeb Abdul, kwa jina lengine, 'Diamond Platnumz', anaendelea kujizolea sifa kimataifa baada ya kushinda tuzo tatu za Channel O African Music Awards.
Tamasha lilifanyika nchini Afrika Kusini mwishoni mwa wiki.
Diamond alijizolea tuzo tatu, ikiwemo ya mwanamuziki mgeni mwenye kipawa kikubwa, mwanamuziki bora zaidi kwenye mtindo wa Afro-Pop na tuzo ya mwanamziki bora zaidi katika kanda ya Afrika Mashariki.
Hii ni mara ya pili mwaka huu kwa Diamond kujinyakulia tuzo za mwanamuziki bora
Diamond anajulikana kama mwanamuziki anaeenziwa zaidi nchini Tanzania na alishinda tuzo hizo kwa wimbo wake 'Number One', na kuwabwaga wanamuziki wengine wanaosifika kikanda na kimataifa.
Hii ni mara ya pili mwaka huu kwa Diamond ambaye mwezi Mei alishinda tuzo saba katika mashindano mangine ya wanamuziki ikiwemo mwanamuziki bora zaidi wa kiume , mwandishi na mtunzi bora zaidi wa nyimbo pamoja na mtumbuizaji bora zaidi Tanzania.
Mwanamuziki Tiwatope Savaga wa Nigeria naye alijinyakulia tuzo ya mwanamuziki bora zaidi wa kike hasa kwa vile alivyoimba kibao chake 'Eminado'.
Tuzo hizo huandaliwa na kituo cha televisheni ambacho hucheza tu muziki cha Channel O.

0 comments:

Post a Comment