Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Friday, April 22, 2016

 
Gazeti la Sunday Times limemtangaza muimbaji Adele kuwa mwanamuziki tajiri wa kike nchini Uingereza,kulingana na Orodha ya wanamuziki 50 mamilionea nchini Uingereza na Ireland.
Mmwanamuziki huyo anatajwa kuwa na utajiri wa pauni milioni 85 akiwa amejiongezea pauni milioni 35 ikilinganishwa na mwaka uliopita.
Adele ameongoza ordha ya wanamuziki wa kike wenye umri wa chini ya miaka 30  mataji nchini Uingereza na Ireland kwa takribani miaka 5
Utajiri wa mwanamuziki huyo uliongezeka kufuatia kutolewa kwa albamu ya 25,ikiwa ni yake ya kwanza baada ya miaka minne.
Mwanamuziki huyo aliorodheshwa wa 9 mwaka 2011,lakini ilipofikia mwaka 2012 alikuwa kileleni hadi kufikia sasa.

0 comments:

Post a Comment