Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Friday, April 22, 2016

 42116-prince-getty-04
Mwanamuziki wa marekani Prince Rogers Nelson,legendary musician aliyefahamika zaidi kwa jina la Prince,ametangazwa kufariki jana April 21 akiwa na umri wa miaka 57.
Mitandao ya kijamii na vyombo vingi vya habari nchini marekani vimetoa ripoti juu ya chanzo cha kifo cha mwanamuziki huyo mahiri kuwa ni kuzidisha utumiaji wa madawa ya kulevya.


Prince pia aliahirisha matamasha mawili ya ziara yake ya muziki aliyoipa jina Piano & A Microphone Tour ,la kwanza lilikuwa April 7, 2016, katika ukumbi wa  Fox Theatre huko Atlanta, Georgia, kwa kusema alikuwa anasumbuliwa sana na mafua (flu) badala yake alitumbuiza siku ya tarehe 14,japo pia alikuwa hajisikii vizuri kabisa.
Asubuhi yake iliripotiwwa mwanamuziki huyo kuamuru kutua kwa dharula ndege binafsi aliyokuwa akisafiri nayo kuelekea Mineapolis kitendo kilichopelekea kutumbuiza siku moja baadaye tamashani.
Watu wa karibu wa Prince waliwahi kusema Prince amekuwa akisumbuliwa na "bad dehydration" ia imekuwa ikimsumbua wiki kadhaa japo ripoti ya madaktari inasema walimhudumia kama mtu aliyezidisha madawa ya kulevya.
Siku mbili kabla ya kifo chake,Prince alihudhuria tamasha la Lizz Wright katika ukumbi wa Dakota Jazz Club April 19.[150]
Prince alikutwa amefariki katikalifti ( elevator) asubuhi ya April 21, 2016 nyumbani kwake huko Paisley Park complex.
Watu waliomuona mida ya saa tatu na dakika 43 asubuhi walipiga simu ya dharula na hata walipofika watoa huduma na kumfanyia huduma ya  CPR, haikumuamsha na baadaye saa nne na dakika 7 alifariki.
Kufuatia vyombo vya habari watu mashuhuli kama U.S. President Barack Obama walionesha kuhudhunishwa walitma salamu za rambi rambi ,wengine wanamuziki na mastaa mbalimbali kama Demi Lovato, Katy Perry, Frank Ocean, Brian Wilson, Missy Elliott, Madonna, Justin Timberlake, Questlove, Mick Jagger, Paul McCartney, Simon Raymonde, Chaka Khan na wengine wengi ambapo katika majengo na madaraja mbalimbali wamewasha mishumaa ya rangi ya dhambarau kama ishara ya maombolezo kwa mwanamuziki huyo.
Timu ya Dj show inasikitika kwa kifo cha mwanamuziki huyo mahiri na tuasikitika pia kutoa taarifa kwamba pamoja na mwanamuziki Princekuwa na nyimbo nyingi zilizofanya vizuri katika chati kubwa kubwa za muziki kama  Billboard Top 40 hits na kuwa mwanamuziki wa kwanza kusambaza muziki wake mitandaoni kutotunukiwa nyota ya heshima ( star on the Hollywood Walk of Fame......),
The Hollywood Chamber of Commerce,ambao ndiyo wanasimamia mchakato huo kupitia msemaji wake Walk of Fame spokeswoman Ana Martinez wamethibitisha kuwa kweli hawajamuwekea nyota hiyo ya heshima Prince ambaye real name ni Prince Rogers Nelson , tu kwasababu jina lake halikuwahi kupendekezwa wala kupigiwa kura kwa mchakato huo.

0 comments:

Post a Comment