Kufuatia tukio la hivi karibuni la kumshambulia mtu mmoja huko Washington Dc na kufikishwa polisi,muimbali mahiri wa muziki wa R&B na pop,Chris Brown,ameamua kwenda kujiandikisha katika kituo cha mafunzo mbalimbali maalumu ( Rehab) kwaajili ya kujifunza kukabili na kujicontrol pindi inapotokea kuchukizwa na lolote.
cnn.com imeripoti kwamba jaji anayeeshikilia kesi anaweza kumfunga Chriss Brown miaka isiyopungua minne kwa kosa la kumshamulia Rihanna ikiwa atakutwa na makosa ya moja kwa moja ya kumshambulia mtu huko Washington Dc hivi karibuni,sababu ni Brow atakuwa kavunja sheria kwa bado yupo katika uangalizi kufuatia tukia la kumshambulia Rihanna miaka miwili iliyopita.
Rehab kazi yake ni kumrudishia mtu hali yake ya kawaida ikiwa atakuwa mlevi kupindikia,mteja wa madawa ya kulevya,afya kutetereka kwa sababu mbalimbali,matatizo ya kifedha,kuachwa,kufukuzwa kazi nk.
Wakati hayo yakiendele Mike Tyson anahofia maisha ya Chris Brown ,akiongea katika mahojiano na 95.5 PLJ Morning Show asubuhi ya leo,amesema,Chriss Brown asipobadilika na kuacha hizi tabia,itamgharimu sana na ni wazi anailazimisha jela.
Wednesday, October 30, 2013
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment