Muimbaji maarufu wa muziki wa R&B,Chris Brown amejikuta mikononi mwa polisi wikiendi hii baada ya kumshambulia mtu mmoja huko Washington,DC.
Myandao wa TMZ unaripoti,ilikuwa majira ya saa 10 alfajiri Chriss Brown alibishana na mtu mmoja nje ya W Hotel na baadae kumpa makonde ya uso na inasemekana mjeruhiwa huyo hakujibu shambulizi
Mtu huyo aliyejeruhiwa ambaye si mshabiki wa Brown amesema,yeye na rafiki yake walikuwa wakipiga picha basi la ziara la Chriss Brown,wakatokea wadada wawili waliotaka kuingia kwa basi hilo wazauliwa mlangongi,wakati jamaa wanaendelea kuchukua piacha ndipo Chriss Brown alipoanza kuwarushia maneno machafu na baadae kumshambulia mmoja wao kwa makonde ya usoni kitendo kilichopeleka kuteguka pua ya jamaa.Taarifa zaidi zinadai jamaa alipelekwa hospitali na alitakiwa kufanyiwa upasuaji waharaka.Baada ya tukio Chris na bodyguard wake walipolekwa polisi ambapo dhamana haikuwa wazi mpaka watakaposomewa mashitaka leo jumatau.
Ikumbukwe Chriss Brown bado yupo chini ya uangilizi kisheria tangu ampige Rihanna.
Habari zaidi zinadai,ikiwa Chriss Brown atakutwa na makosa moja kwa moja anaweza kukutwa na adhabu ya kifungo kisichopungua miaka 4 gerezani.
Monday, October 28, 2013
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment