Mwanariadha wa Afrika Kusini anayekabiliwa na kesi ya
mauaji, Oscar Pistorius, amedaiwa kuhusika katika malumbano ndani ya
klabu moja nyakati za usiku mwishoni mwa wiki.
Mwanariadha huyo alikuwa katika klabu moja
alipojikuta katika hali ya majibizano makali na mfanyabiashara mmoja
aliyekuwa amemuuliza kuhusu kesi anayokabiliwa nayo.Tukio hilo lilitokea katika klabu ya kifahari mjini Sandton kufuatia madai kuwa Pistorius aliwatusi marafiki wa Jared Mortimer pamoja na kuitusi familia ya Rais wa Afrika Kusini Jaocb Zuma.
0 comments:
Post a Comment