Kufuatia ushindi huo Ujerumani walinyakua taji la nne la dunia.
Kipa wa Ujerumani Manuel Nuer alitawazwa kuwa kipa bora na akatuzwa ''Golden Glove''.
Ijapokuwa alishindwa kutwaa ubingwa wa dunia Lionel messi alitawazwa kuwa Mshindi wa tuzo la ''Golden Ball''.
Kufuatia ushindi huo,Ujerumani wanakuwa ndiyo timu ya kwanza kupokea zawadi kubwa ya kitita cha fedha kuwahi kutokea katika historia ya kombe la dunia,wamepatiwa dola millioni 35.
Argentina ndiyo washindi wa pili wamejipatia dolla millioni 25,Netherlands ewashindi wa tatu na wamejipatia dolla millioni 20 wakifuatiwa na washindi wa nne Brazil dolla millioni 18.
Makala yajayo ya kombe la dunia yataandaliwa nchini Urusi mwaka wa 2018.
0 comments:
Post a Comment