Bbc.co.uk/swahili/habari/2014/10/141030imeandika,Katika utafiti uliochapishwa katika jarida la saratani,Watafiti
kutoka chuo kikuu cha Montreal wamebaini kwamba ikilinganishwa na
wanaume walio na mpenzi mmoja katika maisha yao yote,kulala na zaidi ya
wanawake 20 kunapunguza uwezekano wa kupatikana na ugonjwa huo kwa
asilimia 28.
Wanaume 3,208 walishiriki katika utafiti huo ambapo kati yao Wanaume
1,590 walipatikana na ugonjwa huo kati ya Septemba mwaka 2005 na Agosti
mwaka 2009.
Kwa jumla watafiti hao walibaini kwamba wanaume wenye saratani ya
kibofu cha mkojo kuna uwezekano mara mbili kwa wao kuwa na watu wa
familia zao wenye saratani.
Hatahivyo ushahidi unaonyesha kwamba idadi kubwa ya wapenzi wa kike miongoni mwa wanaume inapunguza tishio la ugonjwa huo.
Mwanamume anapojamiana na zaidi ya wanawake 20 katika maisha
yake,tisho la kupata ugonjwa huo linapoungua kwa asilimia 28 mbali na
asilimia 19 kwa aina yoyote ya ugonjwa wa saratani.
Utafiti huo pia umebaini kwamba mmoja kati ya wanaume wanne wa kiafrika hupatikana na saratani
Thursday, October 30, 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment