Ile vita ya maneno baina ya rappa Snoop Dog na rappa wa kike Iggy Azalea immendelea kupamba moto.Baada ya Snoop dogg kuweka picha ya mdada albino katika instagram na kuandika Iggy akiwa hajajipodoa,na Iggy kumchana Snoop na kusema huwa anawatuma walinzi kumuomba wapige picha ya pamoja,vita imeshika sura nyingine,mara hiirappa Snoop Dogg amemfananisha Iggy Azalea na waigizaji wa filamu ya White chicks ya Marlon Wayans.
Naye rappa mkonmgwe toka kundi la Dogg Pound,Daz ameingilia mzozo huo kwa kusema,Iggy Azalea inabidi ajitambue nafasi yake katika ulimwengu wa rap,ni msanii mdogo sana kuanza kuzusha mabeef na miamba ya rap kama Snoop.
Daz
pia ameongeza kusema rappa Snoop hajali lolote kuhusu Iggy sababu si wa level zake na zile picha aliziweka kama mzaha wa kawaida tu. .
Naye rappa Snoop amemuita Iggy muongo na mzushi baada ya mdada huyokudai Snoop huwa anawatuma walinzi kumuomba wapige picha ya pamoja.
Tazama picha aliyoweka rappa Snoop ya kumfananisha Iggy na muigizaji wa filamu ya White chicks:
Wednesday, October 15, 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment