Mashabiki wa muziki wa rappa Tyga wnatakiwa kuwa na subira kwani tarehe ya kuzindulliwa albamu ya rappa huyo ya ''The Gold Album: 18th Dynasty,imeahirishwa.
Albamu hiyo ya nne ya rappa Tyga ilipangwa kuzinduliwa tarehe 27 Jan kupitia lebo yake ya Last Kings chini ya Cash Money lakini tarehe imeahirishwa na haijatajwa itazinduliwa lini.
Kufuatia kucheleweshwa huko,rappa Tyga amezipeleka lawama katikalebo yake ya Cash Money.
Tyga yupo matatani na ametangaza kutaka kujitoa katika lebo ya YMCMB na amemtuhumu bosi wa lebo hiyo kuwa anamshikilia mateka.
Tyga kwasasa yupo katika mchakato wa kuisukuma na kuitangaza albamu yao ya pamoja na Chris Brown, Fan of a Fan 2, ambayo imepangwa kuzinduliwa miezi ya karibuni na tayari washaachia wimbo ''Ayao'' na kuufanyia video.
Tyga atajiunga na Chris Brown na Trey Songz katika ziara ya muziki waliyoipa jina “Between the Sheets Tour,” ambayo itaanzia hukoHampton.
Lebo ya Cash Money imekuwa katika utata na wasanii wake ambao wengi wamekuwa wakilalamikia uongozi kwa matatizo mbalimbali.Li Wayne ametangaza kujitoa,Busta Rhymes alivunja mkataba baada ya kuwa katika lebo kwa miaka miwili bila kufanya albamu,wengine ni Bow Wow ambaye alisajiliwa na lebo hiyo mwaka 2009 lakini mpaka hii leo hajafanya albamu.
0 comments:
Post a Comment