Usiku wa kihistoria katika muziki unazidi kunogeshwa. Usher, Pharrell Williams, Common, John Legend, na Sam Smith wameongezwa katika orodha ya wanamuziki watakaotumbuiza katika sherehe za 57 za utoaji wa tuzo zaGrammy.
Mshindi mara 8 wa tuzo hizo za Grammy na aliyetajwa kuwania tuzo hiyo mara nne katika tuzo za mwaka huu,Usher atashambulia jukwaa huku mtajwa kwa mara ya kwanza katika tuzo hizo aliyetajwa kuwania tuzo mara 6 mwaka huu,muimbaji wa uingereza,Sam Smith,naye atatumbuiza.
Sambamba na Usher na Sam Smith,Pharrell,ambaye pia ametajwa kuwania tuzo hizo mara sita naye atatumbuiza.
Common na John Legend wataungana jukwaani kutumbuiza wimbo wao “Glory”,mbali na kutumbuiza,Common ametajwa kuwania tuzo za Best Rap/Song Collaboration kwa wimbo “Blak Majik” na Best Rap Album kwa albamu Nobody’s Smiling.
Wengine watakaotumbuiza katika sherehe za 57 za utoaji wa tuzo hizo kubwa kabisa duniani za Grammy zitakazoongozwa na rappa LL Cool J ni sambamba na Madonna, Ariana Grande, Ed Sheeran, Miranda Lambert, AC/DC na Eric Church.
Tamasha la utoaji wa tuzo za Grammy mwka huu zitafanyika siku ya jumapili tarehe 8 mwezi Febkatika ukumbi wa Staples Center huko Los Angeles.
0 comments:
Post a Comment