Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Wednesday, March 25, 2015

Chris Brown Baby Mama
Wanamuziki na wasanii wengi wamekuwa katika mtindo wa kuwatenga na kuwatelekeza mama na watoto,lakini hii imekuwa tofauti kidogo kwa mwanamuziki Chris Brown kwani ametamka kutaka kuwasogeza mama na mtoto pande za Hollywood Hills ili awe karibu nao na amlee binti yake.

Mtandao wa TMZ umeandika,mama wa mtoto huyo ambaye ni Nia Guzman,31mwenyeji wa old Houston amesema Chris Brown anajivunia kuwa baba wa binti huyo wa miezi 9,kwa kusema yupo nao karibu na anafuatilia kuhusu mtoto mara kwa mara.Royalty na mama yake watahamia huko L.A ili kuwa karibu na baba wa mtoto kwani wanaishi umbali wa takribani km 1372 kutoka mji anapoishi Chris Brown.
Taarifa zaidi zinasema,Chris anatoa pesa ya matumizi na mahitaji ya mtoto zaidi ya ile waliyokubaliana.

0 comments:

Post a Comment