Busta alitangazwa kusainiwa na Cash Money mwezi November mwaka 2011.
Baada ya miaka miwili,Busta Rhymes sasa amejitangaza si mwana YMCMB tena.
Busta Rhymes ameyasema hayo alipokuwa anahojiwa katika kipindi cha SiriusXM asubuhi kupitia 0MTV News,huk akidai ameondoka salama hakuna bifu wala tatizo lolote ila ni mambo ya kiubunifu na maswala ya kikazi japo amekaa YMCMB miaka miwili bila kuachia albamu hata moja.
Busta anasema alipofikia uamuzi huo alimjulisha kiongozi wa kundi hilo,Birdmannaye akaridhia.
Busta hivi karibuni ameachia singo “Calm Down” feat Eminem ambayo itapatikana katika albamu yake ya 10, E.L.E. 2.
Thursday, July 24, 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment