Mwezi uliopita star wa G-Unit,Tony Yayo alipost picha ya Remmy Ma na ujumbe Free Remmy Ma katika Instagram na kumshawishi bosi wa G-Unit,50cent kumsaini mara tu rappa huyo aliyewahikuwa katika kundi la,Terror Squad,Remy Ma.
Remy Ma baada ya kutoka jela amefanya mahojiano ya kwanza ya radio na mtangazaji wa kituo cha power 105.1 na hiki ndicho alicho kisema : Sipo tayari kusainiwa na lebo yeyote kwasasa,nahitaji muda wa kuangalia mambo kwani naona kuna mabadiliko sana katika sanaa hii,kuhusu Nicki Minaj alisema, Nick amekuwa nami karibu hata nilipokuwa kifungoni,anafanya vema katika sanaa ila ningependa kuona wengine wengi wanafanya kama yeye na si kumwachia uwanja atambe.
Remy Ma amewashukuru sana rappa "50 ambaye amekuwa akimwandikia barua za kumfariji na kumpa moyo wakati wote na Keyshia Cole.
Remy Ma pia ameongea kwamba hana bifu na kiongozi wa Terror Squad Fat Joe.
Wednesday, July 23, 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment