Katika kesi iliyosomwa jana (July 10) hakimu wa mahakama ya New York amemtaka rapa 50 Cent ambaye hakufika mahakamani kumlipa dolla millioni 5 mama mtoto wa kike wa rapa Rick Ross ikiwa ni adhabu kwa kumdhalilisha na kukiuka taratibu za haki za binadamu dhidi yake ambapo kwa kila kosa ametakiwa kulipa kiasi cha dolla millioni 2.5.
Mama huyo wa binti wa rappa Rick Ross anayetambulika kwa jina la Lastonia Leviston,alifungua kesi katika mahakama ya New York City kumshitaki rappa 50 Cent kufuatia kufuatia 50 kusambaza mkanda mchafu wa mama huyo katika mitandao.
Wakili wa Leviston,Philip Freidin amesema rapa 50 Cent alijiingizia pesa nyingi kupitia mkanda huo mchafu aliousambaza katika mitandao,tarifa zaidi zinadai mkanda huo umetizamwa na watu zaidi ya millioni 3 katika mtandao wa YouTube.
Saturday, July 11, 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment