Star wa Rnb Chris Brown amekuwa gumzo katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii baada ya kutuma picha na ujumbe akiomba kupatiwa msaada aweze kuondoka nchini ufilipino baada ya kuzuiwa kuondoka nchini humo.Taarifa zaidi zinasema,Chris Brown alienda nchini Philipines kutumbuiza katika tamasha lililofanyika juzi na baada ya tamasha hilo Brown alijipanga kuondoka nchini humo kesho yake kuelekea Hong Kokng kuendela na ziara yake ya muziki ndipo maafisa wa usalama walipomzuia kwa kile walichosema ana deni analotakiwa kulilipa nchini humo kutokana na kutofika katika tamasha alilolipwa ili atumbuize katika sherehe za mwaka mpya na hakutokea.
Chris Brow ametumia mtandao ya kijamii kuomba msaada kwa viongozi wa Marekani akimtaja hadi raisi Obama ili aweze kuruhusiwa kuondoka nchini Philippines.
Friday, July 24, 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment