Leo zimetimia siku 10 tangu ma rapa Drake na Meek Mill kukwaruzana na kurushiana madongo baada ya rapa Meek Mill kumchana Drake katika mitandao ya kijamii na jukwaani kwamaba anaandikiwa nyimbo zake.
Drake alijibu mapigo siku mbili baadaye kwa kuachia wimbo wa kumdiss Meek Mill alioupa jina ''Charged Up'' na siku mbili baadaye akaachia diss track nyingine aliyoipa jina ''Back To Back'' nyimbo ambazo rappa Meek Mill hakujibu mapigo bali alizibeza diss track hizo kwa kuziita ''soft like baby lotion.
Ikiwa ni siku 9 zimepita tangu kuanza beef hiyo na rapa Meek Mill kuonekana kama amsehindwa kujibu mapigo,jana ( July 30 ) Meek Mill alijibu mapigo na kuvunja ukimya kwa kuachia diss track aliyomshirikisha Quentin Miller ambaye anatajwa kumwandikia Drake nyimbo,track aliyoipa jina "Wanna Know" katika kipindi cha dj mkongwe marekani Funkmaster Flex ndani ya Hot 97.
0 comments:
Post a Comment