Baada ya kuonekana kumuunga mkono Tennis star Serena Williams kwa
kumshanglia kwa nguvu katika mashindano ya mpira wa tennis ya U.S Open
hivi karibuni,rappa Drake kwa mara nyingine ameoneka kumuunga mkono
Serena baada ya kuhudhuria na kukaa siti za mbele kabisa katika
maonyesho ya mitindo ya mavazi ya Serena Williams ikiwa kama sehemu ya
maonyesho ya New York Fashion Week jana siku ya jumanne.
Wanamitindo
walitembea jukwaa huku katika spika zikisiskika nyimbo mbali mbali za
Drake zikiwemo “Hotline Bling,”“My Love” na “Ojuelegba,”
aliyoshirikikishwa na msanii toka Africa,mnaijeria Wizkid.
Drake pia alionekana akiwa na Serena backstage akimpongeza kwa furaha na mabusu mkononi.
Drake pia alionekana amekaa siti za mbele na Anna Wintour ambaye ni editor in chief wa jarida la Vogue baadaye picha hiyo ikatumwa mtandaoni ikiwa na caption “Me and bae.”
Wednesday, September 16, 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment