Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Friday, September 4, 2015

 
Beyoncé Giselle Knowles (alizaliwa 4 Septemba 1981), anayefahamika zaidi kwa jina moja Beyoncé pronounced /biˈjɒn.seɪ/ ni mwimbaji wa R & B, mtunzi wa nyimbo, mtayarishaji wa rekodi, mwigizaji na mwanamitindo kutoka Marekani. Alizaliwa na kukulia Houston, Texas na alihudhuria shule mbalimbali zinazofunza sanaa. Pia alianza kushiriki katika mashindano ya kuimba na kucheza ngoma akiwa mtoto. Knowles alikuja kujulikana katika mwisho wa miaka ya 1990 kama mwimbaji kiongozi wa kikundi cha wasichana cha R & B, Destiny's Child. Kulingana na Sony, mauzo ya rekodi za Knowles, yakiunganishwa na yale ya kikundi cha Destiny's Child, yamezidi milioni 100.[1]
Wakati wa kuvunjika kwa kikundi cha Destiny's Child, Knowles alitoa albamu yake ya kwanza, Dangerously in Love (2003), ambayo ilikuwa mojawapo ya albamu za mwaka zilizokuwa na mafanikio zaidi na jambo hili liliashiria uwezo wake wa kufaulu kama msanii kivyake. Albamu hiyo ilikuwa na mafanikio muhimu ya kibiashara, huku ikitoa nyimbo mashuhuri kama "Crazy in Love", "Baby Boy", na kumshindia Knowles tuzo tano za Grammy katika mwaka 2004. Kutawanyika kwa kikundi cha Destiny's Child mwaka 2005 kuliendeleza mafanikio yake: albamu yake ya pili, B'Day, iliyotolewa mwaka 2006, ilikuwa namba moja kwenye chati za Bango, na ilikuwa na nyimbo kama "Déjà Vu", "Irreplaceable", na "Beautiful Liar". Albamu yake ya tatu, I Am... Sasha Fierce, ilitolewa Novemba 2008, na ilikuwa na nyimbo kama "If I Were a Boy", "Single Ladies (Put a Ring on It)", "Halo" na "Sweet Dreams". Knowles amefikisha idadi ya nyimbo tano zinazopendwa sana miongoni mwa orodha ya nyimbo 100, hivyo basi kuwa mmoja kati ya wasanii wawili wa kike walio na idadi kubwa ya nyimbo zilizochukua nafasi ya kwanza katika miaka ya 2000.
 Mafanikio ya albamu alizoimba akiwa peke yake yamemfanya Knowles kuwa mmoja wa wasanii wanaosifika sana katika sekta ya muziki, na amepanua kazi yake kwa kujihusisha na uigizaji na kuidhinisha bidhaa. Alianza kazi yake ya uigizaji mwaka 2001, aliposhiriki katika filamu ya kimuziki [4] Katika mwaka wa 2006, alishiriki kama mmoja wa wahusika wakuu katika filamu ya malinganisho ya 1981 ya Broadway musical Dreamgirls, ambayo ilimfanya ilimpatia uteuzi mara mbili katika Golden Globe Nominations. Knowles alizindua shirika la familia yake la mitindo, House of Deréon, mwaka 2004, na limekuwa likihusika na kuidhinisha bidhaa kama Pepsi, Tommy Hilfiger, Armani na L'Oréal. Katika mwaka wa 2009, jarida la Forbes lilimworodhesha Knowles namba nne katika orodha yake ya watu mashuhuri walio na nguvu na ushawishi mkubwa katika dunia, wa tatu katika orodha ya wanamuziki wa hadhi ya juu, na namba moja katika orodha ya juu ya watu mashuhuri wanaolipwa malipo bora zaidi chini ya miaka 30, akiwa na zaidi ya mapato ya dola milioni 87, kati ya 2008 na 2009

0 comments:

Post a Comment