Lil Wayne na Birdman mbioni kumaliza matatizo na tofauti zao.
Mtandao wa story za kidaku za mastaa wa America,TMZ,umeripoti kwamba raisi wa Young Money, Mack Maine aliwaunganisha kwa simu rappa Wayne na Birdman masaa kadhaa kabla hawajakutana katika parti ya mwka mpya iliyoandaliwa na Drake, huko Miami.
Mtu wa karibu na wawili hao amesema waliongea maswala kadha yakiwemo ya kumalizana madeni ya mamilioni ambayo Birdman anadaiwa na Wayne.
Mack Maine anaelekea kufanikisha kazi ya kumaliza tofauti kati ya Weezy na Baby,na katika kuuthibitishia uma aisi huyo wa Young Money alipost picha mitandaoni na kuandika ujumbe huu:
“United We Stand Divided We Fall!!”
0 comments:
Post a Comment