Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Saturday, September 3, 2016

 1998 Chris Tucker na Jackie Chan wakiigiza katika Rush Hour mwaka1998.
Muongazaji na mwigizaji mashuhuri wa filamu Jackie Chan atapokea tuzo ya staha ya Oscar kwa mchango wake mkubwa katika tasnia ya filamu.
Jopo linalotoa tuzo za Oscar pia limeidhinisha kutuzwa kwa mhariri Anne Coates, mwelekezi Lynn Stalmaster na mwandalizi wa filamu za makala Frederick Wiseman.
Rais wa jopo hilo Cheryl Boone Isaacs amewataja wanne hao kama "waasisi halisi na stadi katika kazi waliyoifanya".
Chan, 62, alikuwa mwigizaji nyota katika filamu nyingi za kung-fu zilizoandaliwa katika nchi yake ya kuzaliwa, Hong Kong.
Alivuma kimataifa kwa filamu kama vile Rumble in the Bronx, Rush Hour na filamu ya vibonzo ya Kung Fu Panda.
Jack Chan pamoja na umahiri wake waote hajawahi kupatiwa tuzo ya Oscar.

0 comments:

Post a Comment