Kanye West amepamba vichwa vya habari katika magazeti na hata mitandao ya kijamii baada ya kumtembele raisi mteule wa Marekani Donald Trump katika jengo lake la Trumo Tower huko Manhattan jana ashubuhi (Dec. 13).
Kanye West akiwa katika muonekano wa mtindo mpya wa nywele ''blonde'' hapo mwamnzo alipoulizwa nini sababu ya kukutana na waliongea nini na Trump aligoma kuwajibu waandishi wa habari lakini aliwasisitiza wampige picha kaiwa na raisi huyo.
Baada ya kuwaacha watu na sintofahamu Kanye West aliweka bayana sababu ya mkutano wake na Trump na waichojadili kupitia akaunti yake ya twitter kwa kusema:nilitaka kukutana na rais mteule ana kwa ana bila ya kuwa na watu wa kati ili kumuelezea changamoto zilizopo mitaanina na zinazowakabili watu muhimu kama walimu na kumuelezea hali ya vitendo vya mauaji vinavyoendelea katika mitaa ya Chicago na kusisitiza kusema kama kweli tunahitaji mabadiliko inahitajika tumuunge mkono raisi huyo mteule.
Hii si mara ya kwanza kwa Kanye West kuonyesha anamuunga mkono Trump kwani akiwa katika moja ya maonyesho yake katika ziara yake ya Saint Pablo Tour aliwahi kusema kama angepiga kura angempigia Trump.
Wednesday, December 14, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment