Taarifa mpya zimetufikia kuhusu kuvunjika kwa mahusiano ya mastaa wa rap Nicki Minaj na Meek Mill.
Mtu wa karibu na mastaa hao amesema anaamini sababu kubwa iliyopelekea Nicki Minaj na Meek Mill kumwagana ni kile kilichotokea walipoenda kusherekea birthday ya Nicki huko katika visiwa vya Turks and Caicos mapema mwezi December.
Taarifa zaidi zinasema Minaj hakufurahishwa na kitendo cha Meek kutompatia muda zaidi ya kuwa naye na kuwa zaidi na washakaji zake kitendo kilichosababisha Nicki kumchana ndipo Meek alipokasirika na kumuondoka na kumuacha Nicki visiwani humo .
Hiyo inatajwa kuwa ndiyo sababu kubwa japo kuna minong'ono kwamba Meek amekuwa akichepuka na mrembo anayefahamika kwa jina la Sonye Rasool japo mrembo huyo alipoulizwa amekanusha.
Nicki ndiye aliyethibitisha kuvunjika kwa mahusiano yake na Meek kwa kuandika “I am single,” “Focusing on my work & looking forward to sharing it with you guys really soon. Have a blessed New Year. Love u.”kupitia ukurasa wake wa tweeter.
0 comments:
Post a Comment