Muimbaji mahiri wa aina ya muziki wa Dancehall Patoranking asema alianza safari ya muziki huyo kama mcheza shoo ali[pohojiwa na mtangazai wa televisheni huko Jamaica alipoikwenda kuitangaza albamu yake.
Akiongea na mtangazaji wa Onstage TV, Patoranking pia ameongelea nguvu ya muziki wa Afrobeat Africa na duniani kote.
Kama ilivyo kwa baadhi ya mastaa wa muziki wa bongo flava hapa bongo kama Shetta,Msamy wamewahi kukiri kuanza kama wacheza shoo kwa mastaa wengine,Patoranking amesema haikuwa rahisi kufika hapo alipo na kuwa king wa muziki aina ya dancehall Afrika,Pato amesema alikuwa anaupenda sana muziki wa ragga dancehall na akaona namna pekee ya kujisogeza kwa watakaomsadia na kutimiza ndoto zake ni kuchagua kazi itakayompatia njia,hivyo akaamua kuwa mcheza shoo...
Pato pia ameongelea anavojiona amefanikiwa na mashabiki wanavompokea na kumpa chachu ya kufanya vizuri zaidi mpaka kuzindua albamu lake ya "God Over Everything".
Alipoulizwa kwanini hakwenda ulaya na marekani kuanza mishe za muziki alijibu "It is Africa, charity begins at home, if it's not big at home, it won't be big abroad."
0 comments:
Post a Comment