Hit maker wa ngoma kama Walaghai,Uaminifu,Aza nk amefunguka na kusema awezi kufanya muziki wa Hiphop wala haitaji kutajwa kama mwanamuziki wa muziki huo kwa kile alichokisema hataki kuchelewa.
Akiongea na Dj Sho ya Radio One msanii Bonge la nyau amesema yeye anafanya muziki wa bongo flava japo katika mtindo wa rap ambayo si ngumu.
Bonge la Nyau ameongeza kusema hatojali kama wana hiphop watamtenga ama kumsema vibaya kama ilivyotokea kwa wengine na kusema yeye anachojali ni kuwashika mashabiki na kufanya muziki mzuri na auze na ajitangaze.
Bonge la Nyau pia ametaja orodha ya ma rapa na wanahiphop anaowakubali kwa sasa ambapo amewataja Mr Blue,Young D,Darasa,Fid Q na Chidy japo amejitoa kwenye reli.
Tuesday, January 31, 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment