Ikiwa ni siku moja tangu Drake kuchafuliwa na habari mbaya ya model wa kike kudai ana ujauito wake,rapa huyo mcanada ameingia tena katika vichwa vya habari baada ya mwanamke mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 24 kuingia nyumbani mwa star huyo bila tarifa wala ruhusa ya walinzi.
Mwanamke huyo alikutwa akijiachia katika moja ya vyumba anavyolalaga Drake akiwa amevalia nguo ya rappa huyo na baada ya uchunguzi kufanyika imegundulika hajaiba chochote zaidi kukata kiu yake kwa kunywa soda mbili na maji
Watu wa usalama walipofika mwanamke huyo aliongopa kwa kusema yumo humo kwa ruhusa maalumu ya wahusika na alipoulizwa nani alipata kigugumizi.
Mwanamke huyo amefunguliwa mashtaka ya uvamizi nyumbani mwa mtu na wizi.
Katika habari nyingine inayomhusu Drake ni kuhusu model Layla anayedai ana ujauzito wake kwa mba habari hiyo ni ya uzushi na mwanamke huyo alifanya kwa kutaka umaarufu haswa mitandaoni mambo yake yaende.
Akithibitisha uzushi wa model huyo,Dj wa Drake DJ Spade ameanika mitandaoni chating zake na model huyo akithibitisha kuzusha ili apate umaarufu ajiingizie kwanja.
0 comments:
Post a Comment