Mtu mmoja mkazi wa Mississippi anayefahamika kwa jina la Kenny Bryant, amemfungulia mashtaka R&B superstar R. Kelly kwa kile alichokidai ana mahusiano na mkewe na wamemuakiza gonjwa la zinaa.
Katika mashtaka hayo bwana Kenny Bryant ameandika sambamba na kuambukizwa gonjwa la zinaa linalofahamika kama Klamidia pia anaugua upwkeke na ukata ambavyo vyote hivyo amesema vimesababishwa na mahusiano kati ya mkewe bi Childress na R.Kelly.
Bryant amesema mkewe bi Childress aliwahi kukiri kuwa na mahusiano na R Kell kabla ya harusi yao mwezi July 2012 ambapo alikiri mahusiano yao yalianza pale alipohudhuria maonyesho R Kelly na kusitisha mahusiano hayo.
Bw Bryant amesema ilibidi aache azi wahamie Atlanta kutafuta maisha na kuamini mkewe atakuwa mbali na Kelly ambapo haikusaidia kwani mkewe huyo alitoroka kila mara kuhudhuria maonyesho ya RNB Star huyo mpaka kuambukizwa ugonjwa huo ambao mkewe amekiri tena kuupata kwa R.Kelly.
Klamidia ni ugonjwa wa kuambukiza ambao husababishwa na bakteria zinazoitwa na sayansi kama Chlamydia trachomatis.
Ugonjwa huu huwa hauonyeshi dalili za wazi kwa karibia asilimia 75 ya wanawake na asilimia 50 ya wanaume, hivyo maambukizi mengi hushindwa kufahamika mapema.
Kama utaachwa bila kutibiwa katika wanawake, klamidia unaweza kuleta
madhara makubwa kwa afya. Klamidia huaribu tishu za uzazi za mwanamke na
kusababisha uvimbe katika fupanyonga (pelvic inflammatory disease, PID). PID inaweza kusababisha mauvimu makali sana katika fupanyonga, utasa/ugumba au utata katika ujauzito ambao unaweza kusababisha kifo.
Watoto waliozaliwa na mama waliombukizwa klamidia huwa na hatari ya kupata upofu au maambukizi katika mapafu.
Thursday, April 27, 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment