Baada ya kukanusha habari za kumjaza ujauzito na kumkana mwanamitindo aliyefahamika kwa jina la Layla Lace ,mwanamke mwingine ameibuka na kusema ana ujauzito wa Drake.
Mwanamke huyo aliyefahamika kwa jina la Sophie Brussaux amesema ana ujauzito wa miezi mitatu na nusu,tayari ameshaajiri mawakili wawili wamsimamie apatiwe haki ya pesa ya matunzo toka kwa Drizzy .
Bi Sophie Brussaux mapema mwaka huu alionekana akiwa karibu sana na Drake wakati star huyo akifanya ziara nchi za ulaya
Sophie Brussaux anayefahamika kama Rosee Divine amesema anao ushahidi wa kutosha ikiwa ni sambamba na ujumbe mfupi wa Drake akikiri kuwa mhusika wa ujauzito huo huku akimuomba mrembo huyo anyofoe tumbo hilo.
Habari toka kwa watu wa karibu na Drake wamesema,mshikaji wao ameukana ujauzito huo baada ya kuwepo na habari kwamba mrembo huyo alitoka na rapa mwingine wakati huohuo.
0 comments:
Post a Comment