Mahakama ya mjini Los Angels imemuamuru Rob Kardashian kukaa mbali na mama wa mtoto wake Blac Chyna kufuatia madai ya kumshambulia mara kwa mara na migogoro baina yao.
Akitoa hukumu hiyo hakimu wa mahakam ya Los Angeles Commissioner James E. Blancarte amesema amefikia kutoa amri ya Rob kukaa mbali na Balck Chyna baada ya Moderl huyo kufikisha madai ya kushambuliwa mwilini na hata kudhalilishwa mitandaoni ambapo kesi hiyo imetajwa kusikilizwa tena August 8, 2017.
Katika shauri hilo inaonekana Kardashian na Chyna waliwahi kugombana na kutengana December 2016, na tukio kama hili kujirudia April 8, 2017 ambapo hayo yote yalisababishwa na vipigo vya Rob Kardashian kwa Chyna knocking ambapo amedai kupigwa ngumi na hata kugalagazwa chini n hata alipojaribu kujifungia chumbani jamaa alivunja mlango.
Wawili hao wapo katika hali ya ugomvi kufuatia kuanikana mitandaoni siku kadhaa zilizopita.
0 comments:
Post a Comment