JAY-Z na Kanye West bado hawapo katika maelewano mazuri na swla hili linaonekana kumkosesha raha mke wa Kanye bi Kim Kardashian.
Mtu wa karibu na Kim Kardashiana amesema reality star huyo amekuwa akijiongelesha kuwa anakerwa na hali ya Mumewe Kanye West na rafiki yake wa Siku nyingi Jay Z kuwa katika mogogoro ya kikazi na hata urafiki hivyo anaomba kila siku siku wamalizane mambo yawe sawa na warudishe uhusiano wao na hata yeye awe rafiki mzuri wa mke wa Jay Z, Beyonce.
“Kim [Kardashian] anaamini ipo siku JAY-Z na Kanye [West] wataweka mambo yao sawa kutokana na historia ya ukaribu wao haswa kirafiki na kikazi na ameonyesha wazi kwamba atafurahia hali hiyo ikiwa shwari kwani anaamini ni sehemu ya familia yao japo yapo yanayosemwa kwamba urafiki kati ya Kanye West na Jay Z na mkewe Beyonce ulianza kuyumba tangu waoane.
0 comments:
Post a Comment