Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Friday, September 20, 2013

Jay-z-and-beyonce-inaug-22012013
Rappa Jay Z na mkewe Beyoncé Knowles Carter siyo tu wanakimbiza katika kiwanda cha muziki bali hata kwa mkwanja,hayo yamejidhihirisha baada ya kutajwa na Forbes kwamba ndiyo wanamziki wanandoa ambao kwa pamoja wanaingiza mkwanja mwingi zaidi kwa kuingiza kiasi kinachikaribia dola millioni100 million katika kipindi cha mwaka.Rappa Jay Z na mkewe Beyoncé Knowles Carter wote ni wanamuziki ambao kila mmoja anafanya kweli katika sehemu yake.
Project ya Jay Z Watch the Throne ilifika mauzo ya platinum na alifanya ziara ya kutambulisha ambayo ilimuingiia kiasi cha dola millioni1.4 kwa shoo moja huko America. Beyoncé Knowles Carter, ambaye alikuwa na likizo fupi ya uzazi wa mtoto Blue Ivy ambaye alizaliwa mwezi January2012,alirudi kwa kishindo na kufanya ziara aliyoiita Mrs. Carter world tour,ambayo ilimuingizia kiasi cha dola millioni2 kwa shoo.
Nyuma ya Bey na Jay wapo wanandoa Tom Brady and Gisele Bundchen amabo wamewapita kiasi cha dola millioni 15 kwani wawili hao wameingiza dola milioni 80.Nafasi ya 3 imeshikwa na ma star wa movie wanandoa Angelina Jolie na Brad Pitt amabo wameingiza dola millioni  $50.

0 comments:

Post a Comment