Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Friday, May 23, 2014

BBC.CO.UK imeandika,vijana ambao ni mashabiki wa muziki nchini Iran walioiga wimbo maarufu wa mwanamuziki maarufu wa Marekani Pharrell Williams, 'Happy' wamejikuta matatni baada ya kukamatwa na polisi.
Kanda ya video waliyoirekodi wakiiga wimbo huo, inaonyesha vijana watatu na wanawake kadhaa ambao hawakuwa wamejitanda mitandoa, wakicheza densi kwenye barabara za nchi hiyo na kwenye paa za nyumba mjini Tehran.Mkuu wa Polisi, Hossein Sajedinia, alisema kuwa kanda ya video inayoonyesha vijana hao wakicheza, imekiuka maadili ya jamii.Kituo cha televisheni ya serikali kilionyesha vijana hao wakikiri makosa siku ya Jumanne.
Vijana hao wanaosema ni waigizaji wanadai kuwa walihadaiwa kushiriki katika kanda hiyo na watu waliokuwa wanatafuta waigizaji wakisema ulikuwa kama mtuhani kwao.
"waliniambia kuwa wanatengeza filamu na kuwa walikuwa na kibali na ndio maana nikakubali kushiriki,'' alisema mmoja wa vijana waliokamatwa.
Mtuhumiwa mwingine alisema walionasa kanda hiyo waliwaahidi kwamba hawataisambaza.
Pharrel aliyeteuliwa kwa tuzo la Oscar kwa wimbo wake huo mwaka huu  alionyesha masikitiko yake alielezea kupitia facebook:"yani siamini kama watoto hawa walikamatwa kwa kujaribu kueneza furaha,'' 
Kanda hiyo ya "Happy we are from Tehran" ilionekana kwenye mtandao wa Youtube tarehe 19 Mei na kufikia sasa imetazamwa mara 40,000.
Chini ya sheria za kiisilamu, sharti mwanamke ajitande kutoka kichwani hadi katika viganja vya mguu.
 

0 comments:

Post a Comment