Rappa toka pande za Miami,Rick Ross ameushtua ulimwengu kwa kupunguza mwili kwa kiasi kikubwa na kubadili muonekano.Ross amepunguza karibia ya pound 200 kwani alikuwa na pound 300 na sasa anakaribia pound 100.
Ross ambaye alishawahi kupoteza fahamu mara mbili ndani ya siku moja kwa matatizo ya afya kutokana na mwili mkubwa,akiongea na waandishi wa habari amesema,amefanikiwa kupunguza mwili kwa kula mlo alioelekezwa,kufanya kazi muda mwingi zaidi na mazoezi.Ross amesema hata afya inahitaji nidhamu.
Ross, 37, amesema anaendelea kufanya kazi za nguvu na muda mrefu haswa katika shughuli zake za kimuziki na hivi karibuni ameachia albamu yake ya saba na ya pili mwaka huu "Hood Billionaire," baada ya kuachia mwezi March albamu ya "Mastermind," ambayo ilifika hadi namba 1 katika chati za Billboard albamu mia 2 bora .
0 comments:
Post a Comment