Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Monday, April 13, 2015

 
Rappa toka pande za St. Louis, Nelly alijikuta mikononi mwa wanausalama baada ya kukutwa na madawa ya kulevya na kiasi kikubwa cha bange jana jumapili  ( April 11 )
Taarifa zidi zinasema,kundi la wanausalama wa mambo ya usafiri na mambo ya ushuru wa mafuta walilisimamisha basi la ziara ya muziki alilokuwamo rappa huyo na baada ya kufanya upekuzi ndipo walipogunduamabegi yaliyokuwa na kiasi kikubwa cha madawa ya kulevya na bangi,silaha mbalimbali zikiwemo handguns,50-caliber Desert Eagle pistol, a .45-caliber Taurus pistol na 500 Smith & Wesson magnum.
Nelly alikamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa makosa ya kukutwa na madawa ya kulevya na bangi na kukutwa na vifuko ambavyo hutumika kwa kuuzia madawa ya kulevya.
Mwanasheria wa Nelly , Scott Rosenblum, ameongea na  CNN na kumtetea mteja wake kwamba,madawa na bangi vilivyokamatwa havimhusu Nelly na kuongeza kusema katika basi hilo kulikuwa na watu 15-20.
Ikiwa rappa huyo atapatikana na hatia adhabu ya kutumikia kifungo ama ya kulipa faini itamkabili.

0 comments:

Post a Comment