Mwana Hip Hop Akon ameamua kutumia pesa zake kusaidia waafrica wenzake.Mtandao wa Eurweb,umeandika Akon ambaye ni raia wa America mwenye asili ya Senegal ametangaza mpango wake wa kuhakikisha waafrica wapatao millioni 600 wanapata umeme.Akiongelea mpango huo mmoja kati ya wamiliki wa mfuko huo bw Said Samba Baithily akiwa sambamba n Akon walisema:“We have the sun and innovative technologies to bring electricity to homes and communities. We now need to consolidate African expertise,” Akon amesema watafungua taasisi maalumu ya kusimamia mpango huo huko Bamako na kuwashirikisha engineers na wafanya biashara wakubwa kuhakikisha wanafanikisha mpango huo wa kusambaza umeme wa Solar Africa.Akon aliongeza kusema,asilimia 70 ya wafrican ni vijana na kwa kufanikisha mpango huu pia itakuwa sehemu ya kusaidia vijana kupata na ajira.
0 comments:
Post a Comment