Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Monday, April 18, 2016

 
DJ Khaled  alidondoka pande za Hot 97 na kupiga stori kadhaa katika kipindi cha Ebro in the Morning. Akiwa katika mahojiano hayo Khaled amefunguka juu ya hali duni za maisha alizopitia mpaka kufikia hapo.
DJ Khaled amesema wakati amehamia Miami aliishi kwa tabu kiasi ambacho ilimlazimu kila mwezi kuhama kwa kufukuzwa kodi na hakuwa na samani zaidi ya masantury yake ya muziki pekee.Ilifika wakati akawa anaingiza kiasi cha dola 100 tu kwa wiki na aliendesha maisha.

Khaled kwasasa anahesabiwa kuwa ni dj na producer mwenye mafanikio makubwa na hivi karibuni amesaini dili kubwa ikiwema na Jay Z na kama haitoshi na Epic.
 DJ Khaled pia ametajwa kuhusika na ununuaji wa hisa zaidi ya asilimia 40 za timu ya mpira wa kikapu inayoshiriki ligi ya NBA ya Miami Heat.

0 comments:

Post a Comment