Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Tuesday, July 26, 2016

 230716052439
Mwanamuziki nguli kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amekamatwa na maofisa wa polisi akiwa nyumbani kwake mjini Kinshasa.
BBC wameripoti Koffi amekamatwa na maofisa wa polisi nchini humo kwa agizo la mwendesha mashtaka.
Koffi Olomide alitimuliwa kutoka nchini Kenya baada ya kipande cha  video kuonekana kuonesha akimpiga teke mchezaji show wake wa kike katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta.
Kofii ilikuwa atumbuiza Kenya siku ya Jumamosi lakini tamasha hiyo ikaahirishwa baada ya Koffi kukamatwa Ijumaa usiku na polisi wa Kenya na siku iliyofuata asubuhi kurejeshwa Kinshasa.
Waandalizi wa tamasha ambayo Olomide alipangiwa kutumbuiza nchini Zambia pia walitangaza kwamba wamefutilia mbali hafla hiyo kutokana na yaliyotokea Nairobi.
Mwanamuziki huyo, akiandika kwenye ukurasa wake wa Facebook Jumapili, aliomba radhi mashabiki wake na hasa “wanawake na watoto”.
“Najutia sana yaliyotokea… kilikuwa ni kipindi kifupi cha wenda wazimu,” aliambia kituo cha tevisheni cha taifa cha RTNC.
Baadaye, aliomba msamaha kutoka kwa raia wote wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambao huenda alihisi kwamba tabia yake iliwakosea heshima.
Waziri wa masuala ya vijana na jinsia Kenya Bi Sicily Kariuki, katika taarifa kwa vyombo vya habari baada ya video iliyoonesha tukio hilo kusambaa, alipendekeza Olomide azuiwe daima kuzuru Kenya.

0 comments:

Post a Comment